advertisement
World Kiswahili Day: Technology Terms In Kiswahili
Shirika la Umoja Wa Mataifa almaarufu United Nations leo yaadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani (SIKIDU) jijini Nairobi na Mombasa. Hii ni maadhimisho ya pili ya siku hii na wadau wanatarajiwa kudhihirisha lugha hii ilivyo sehemu muhimu ya tamaduni na taratibu za Maisha ya kila siku ya Waswahili haswa katika eneo la Afrika Mashariki.
Kama tovuti inayoongelea teknolojia na ukuzi wa teknolojia katika bara la Afrika, CIO Africa leo tunawaelimisha kuhusu vipengele za kiteknolojia na majina yao katika kiswahili. Baadhi ya maneno haya ni vifaa vya teknolojia.
- Artificial Intelligence – Akili Bandia
- Smartphone – Simu Janja
- Cybersecurity – Usalama wa Mtandao
- Internet of Things – Mtandao wa Mambo
- Machine Learning – Kujifunza kwa mashine
- Cloud Computing – Wingu wa utarakilishi
- Laptop – kipakatalishi
- Website – Tovuti
- App – Programu
- Simcard – kadiwia
- Scratch card – kadihela
- Password – nywila
- Keyboard – kicharazio
- Mouse – kiteuzi
- Computer virus – mtaliga
- ATM – kiotomotela
- Flash disk- diski mweko
- Floppy disk – diski tepetevu
- Scanner – mdaki
- Memory card – kadi sakima
Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani
Mwaka huu serikali Kuu ya Kenya imejichukulia usukani kendesha maadhimisho wa siku hii na pia imekuwa mstari wa mbele kufanikisha mipangilio yote. Hii ni tofauti na mwaka uliopita ambapo taasisi mbali mbali za elimu zilijiendeshea maadhimisho ya kwanza ya SIKIDU katika viwango vyao binafsi.
advertisement
Wizara ya Masuala ya Kigeni itakuwa leo Ijumaa na hafla yake katika mkahawa wa QMins ulio mkabala na Bomas jijini Nairobi huku Idara ya Utamaduni na Turathi katika Wizara ya Utalii, Wanyamapori na Turathi za Kitaifa ikishirikiana na Serikali ya Kaunti ya Mombasa kuendesha sherehe nyingine eneo la Fort Jesus Park (Swahili Centre na Swahili Pothub), NMKHTI Grounds, Mombasa.